Skip to main content

Magufuli; Anna Mghwira ana uwezo wa kuchapa kazi.


Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemuapisha aliyekuwa mgombea urais mwaka 2015 Bi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na kusema anaweza kuitekeleza kazi hiyo.
Bi Anna Elisha Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye aliacha kazi.
Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka Bibi Anna Elisha Mghwira kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuondoa kero zinazowakabili wananchi wa Kilimanjaro bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa, dini, makabila na kanda wanazotoka.
Alisema anaamini mwanasiasa huyo ana uwezo wa kutekeleza majukumu yanayoambatana na kazi hiyo.
"Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu, na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro, wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi," amesema Dkt Magufuli, baada ya kumuapisha katika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Bi Mghwira amemshukuru Rais kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na amemuahidi kuwa yupo tayari kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kujenga Taifa.
"Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu, kumekuwa na minong'ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo" amesema Bi Mghwira.
Bi Mghwira alikuwa mgombea pekee wa kike wakati wa kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015.
Amekuwa mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, chama kichanga zaidi Tanzania kilichoundwa 2014.
Mghwira, 56, anatoka mkoa wa Singida. Babake alikuwa diwani na kiongozi chama cha Tanu na baadaye CCM.
Chanzo: BBC Swahili.

Comments

Popular posts from this blog

Korea Kaskazini yaapa kulipiza Kisasi kwa Marekani.

Korea Kaskazini yaionya Marekani kufuatia vikwazo vya UN Korea Kaskazini imeapa kulipiza kisasi na kuhakikisha kuwa Marekani imelipia gharama, kwa kubuni vikwazo vya Umoja wa Mataiafa kufuatia na mpango wake wa silaha za nuklia. Vikwazo hivyo vilivyoungwa mkono kwa kura nyingi na Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi "ni ukiukaji ya uhuru wa nchi," shirika la serikali la habari la Korea Kaskazini KCNA lilisema. Kwa upande mwingine Korea Kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imekataa ombi la kutaka wafanye mazungumzo. Vikwazo hivyo vililenga kuzuia mauzo ya bidhaa za Korea Kaskazini kwa theluthi moja. Uamuzi huo wa Halmashauri ya Usalama wa Umoja wa Mataifa ulitokana na majaribio ya kutupa makombora ya mara kwa mara na Korea ya Kaskazini, jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa wasi wasi kwenye rasi Korea. Katika jibu lake kuu la kwanza Jumatatu, Korea ya Kaskazini imesisitiza kuwa itaendelea kuendeleza mpango wake tata wa silaha za nyuklia. Shirikisho la habari la KCNA lina...

Fahamu namna ya kujitibu/kujikinga kwa mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo: 1. UGONJWA WA MOYO Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo. Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3. 2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ...